Jenerali wa zamani nchini Libya Khalifa Haftar amethibitishwa leo kuwa kamanda mkuu wa jeshi la serikali ya nchi hiyo inayotambuliwa kimataifa.
Hatua hiyo ya uteuzi wa Haftar , mshirika wa zamani wa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi ambaye baadaye alijiunga na vuguvugu la mapinduzi dhidi ya kiongozi huyo wa Libya, unaweza kuweka ugumu katika juhudi za Umoja wa Mataifa kufikia makubaliano kati ya serikali mbili hasimu za nchi hiyo.
Haftar ameunganisha jeshi lake la kawaida na vikosi vya jeshi la serikali upande wa mashariki kupambana na makundi ya itikadi kali ya Kiislamu. Pia amelilenga kundi la Libya alfajiri, ambalo limeukamata mji mkuu Tripoli na kuunda serikali hasimu.